Sunday, November 2, 2014

SOMO LA TATU

    UTUMISHI NA WAJIBU WETU KWA MUNGU    NA WANADAMU

Yaliyomo:

I.Utangulizi

II.Misingi ya Mitume na Manabii.

III.Maana ya Msingi.
(i)Tafakari.
(ii)Mifano ya watu waliojenga Misingi.

IV.Je,Misingi inapitisha nini?
(i)Msingi uliojengwa na Yesu.
(ii)Eliya arejea kwenye Msingi.

V.Tumejengwa juu ya Msingi wa Mitume na Manabii na Yesu Kristo ndiye Jiwe kuu la pembeni.
(i)Mbingu nazo zimejengwa katika Msingi.
(ii)Faida za kujenga kwenye Msingi wa Yesu Kristo.

VI.Mungu ana uwezo wa kuweka Misingi yetu katika mawe mazuri.
(i)Msingi wako umeujenga wapi?

VII.Hatua za kuchukua ili kurejesha Misingi iliyoharibika.
-Toba ya kweli.
-Bomoa Misingi yote iliyopandwa ndani ya Maisha yako.
-Omba.
(i)Rejesha misingi yote ya Baraka maishani ili uweze kusonga mbele.


I.Utangulizi;
''Mtumishi wa Mungu anapaswa  kujitambua na kujiamini kuwa anafahamika kuheshimiwa na aliyemuita.
Jambo jingine muhimu ni kufahamu wajibu wake kwa Mungu  na wanadamu hayo yakizingatiwa kwa uzito unaositahili hapana shaka milango ya Baraka itafunga”


II: Misingi ya Mitume na Manabii.
Mmejengwa katika misingi ya mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni katika yeye jengo lote linaunganishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana.Katika yeye  ninyi nanyi mnajengwa  pamoja kwa maskani ya Mungu katika Roho. Efeso 2:20-22
Vifungu hivi vya maneno vinatuonyesha kuwa tumejengwa juu ya misingi;hii ni wazi kabisa hakuna chochote kisichokua na misingi hapa duniani na mbinguni.Hivyo katika somo hili tunajifunza kuhusiana na misingi mbalimbali ambayo imewekwa na Mungu,iliyowekwa na wazazi,jamaa,uliyojiwekea mwenyewe,madhara na faida,namna ya kutoka tena katika misingi iliyoharibika na mengine mengi.

III:Maana ya  Misingi:
Msingi ni mwanzo wa jambo fulani likiwa ni jema au baya.
Mwanzilishi wa misingi mizuri ni Mungu mwenyewe.
“Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari na juu ya mito ya maji aliithibitisha”
Zaburi 24:2


Ni vyema utambue kuwa katika jambo lolote liwe zuri au baya inategemea misingi imara.
Maandiko yanasema:-
“Kama misingi ikiharibika mwenye haki atafanya nini?”  Zaburi 11:3


Watu wengi wanaposhughulikia matatizo yanapokua magumu kutatulika kwa sababu hawakushughulikia kutoka kwenye misingi,kilichosababisha Eliya aweze kumwita Mungu na moto ukashuka akaweza kukomesha madhabahu za Baali ni kwa sababu alipita katika misingi;maandiko yanatuonyesha kua madhabahu ya Mungu ilikua imevunjika ndio maana madhabahu za Baali zilikua zimepata nguvu.
Hii tunathibitisha katika kifungu hiki cha maandiko kinachosema,
''kisha Eliya akawaambia watu wote,nikaribieni mimi,watu wote wakamkaribia akaitengeneza Madhabahu ya Bwana iliyovunjika” 
1 Wafalme 18:21-30.


Tunaona Mungu hakushuka mpaka Eliya alipojenga Madhabahu,hii ni wazi kua hata Madhabahu ni msingi wa Mungu kwa watu wake;kama Madhabahu ni ya Mungu wako imevunjika hata ungeomba maombi gani Mungu hataonekana wala hatajulikana mpaka utakapojenga Madhabahu hiyo upya.
Kuna watu wengine ambao wanaomba lakini Madhabahu ya Mungu wao ilishavunjika,huwezi ona majibu kamwe.


(i)Tafakari.
Swali:-
Maandiko yanasema wazi misingi ikiharibika,Mwenye haki atafanya nini?
Kama misingi yako ya huduma imevunjika utafanya nini?
Kumbuka kila kilichopo duniani kina misingi yake na ubora wake inategemea ni misingi gani,kuna misingi mingi katika Ulimwengu.
Mfano; kuna misingi ya nchi,ukoo,shule,familia,kanisa,kazi,kilimo,ndoa na mengine mengi.
Kila unachokifanya kiwe ni kizuri ama kibaya ni Misingi.

(ii)Mifano ya watu waliojenga Misingi.
Hawa ni miongoni mwa watu waliojenga Misingi kwenye Biblia.
Mfano wa kwanza;
-Adam
Alifanya dhambi; ule ni  msingi wa dhambi uliojengwa
ulimwenguni ndio maana katika kitabu cha
Warumi 5:12.


Mtume Paulo anasema,''Kwa hiyo kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni na kwa dhambi hiyo mauti na hivyo ikafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi”.
Katika kifungu hiki tunaona dhambi aliyoifanya Adam lakini dhambi hiyo ikatufikia na sisi tusiojua dhambi,ashukuriwe Mungu kwa kutujengea msingi mwingine kama tunavyoona katika kifungu hiki cha maandiko.
''Ndivyo ilivyoandikwa mtu wa kwanza Adam akawa nafsi iliyo hai,Adam wa mwisho ni roho yenye kuhuisha”                                                                               1Wakorintho 15:45


Ukitazama vizuri utaona kilichokua kimekufa kimefanywa hai maana neno huuisha maana yake ni ''fanya hai”,kwa hiyo twaweza sema kwamba Adam wa kwanza ni msingi ulioharibika,Adamu wa pili ambae ni Yesu msingi uliojengwa upya.


Mfano wa pili:
-Abraham
Abraham alizaa na Hajiri ule ulikua ni Msingi wa Baba kuzaa na wasichana wa kazi(Housegirl (s)).Na msingi huo haukupita kwa Isaka badala yake ukaenda kwa Yakobo;Yakobo akazaa na vijakazi wawili wa Lea(Mke mkubwa) na pia wa
Raheli(Mke mdogo).


Nguvu ilimsukuma Yakobo kufanya hivyo ni nguvu ya Misingi ya Babu yake ambae ni Ibrahim.
Pamoja na Ibrahim kufanya makosa hayo kama Misingi mibaya kuna mengine alifanya mazuri yakawa Misingi mizuri kwa mfano:
                 -Alimuamini Mungu hata akahesabiwa haki,huu nao ulikua msingi ulikuwa msingi uliotufikia hata sisi tunaoamini katika Agano Jipya kama tunavyosoma Barua ya Paulo kwa Wagalatia;''kama vile Ibrahim alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki,fahamu basi ya kua wale walio wa Imani hawa ndio wana wa Ibrahim”                                                       
 Wagalatia 3:6-14


Hapa tunajifunza hivi,wenye msingi wa Imani watabarikiwa pamoja na Ibrahimu mwanzilishi wa Msingi huo wa Imani.

Mfano wa 3:
-Daudi
Tunaona pia Daudi alifanya dhambi na dhambi hiyo ilitokana na misingi ilitoharibika,kutokana na uovu wa mama yake kama anavyoeleza katika maandiko haya;''tazama,mimi niliumbwa katika hali ya uovu;mama yangu alichukua mimba hatiani”                                                           
Zaburi 51:5


Yamkini shida iliyopo kwako imetokana na wazazi wako kuweka misingi mibaya au shida ya watoto wako inatokana na misingi mibaya uliyoiharibu mwenyewe;pengine ni huduma yako umeharibu misingi na huduma umeshindwa kuendelea vizuri yapasa kufanya maombi ya kujenga msingi upya kama tulivyokwisha kuona kwa Eliya

Muhimu:
Nchi uliozaliwa yaweza kuwa msingi.
Baba aliyekuzaa naye ni msingi.
Mama aliyekuzaa naye ni msingi.

(IV)Je,Misingi inapitisha nini?
Napenda kila mmoja ajiulize swali la Msingi
Je! Misingi hiyo inapitisha nini maishani mwetu..?
Yale yanayopitishwa na msingi ndiyo matokeo ya maisha yako iwe ni mazuri au mabaya. Hebu jifunze tena katika kifungu hichi cha maandiko “ Neno la Bwana likanijia kusema tena, Mwanadamu uujulishe Yerusalemu machukizo yake. Useme Bwana Mungu huuwambia Yerusalemu hivi; Asili yako         
na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya Mkaanani ; Mwamori alikua baba yako, na mama yako alikua Mhiti. Na katika habari za kuzaliwa kwako siku uliozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala haukuoshwa kwa maji usafishwe; Hukutiwa chumvi hata kidogo wala hukutiwa katika nguo kabisa''  
Ezekiel 16:1-2.



Mungu alipo angalia uovu wa Yerusalem aliona ukitoka katika misingi mitatu;
Moja ,aliona uovu unaotokana na nchi(maana yake ni msingi) ya mkanani;
Mbili ,aliona uovu  wa baba yake ambaye alikuwa Mwamori(neno Mwamori ni msingi)
Tatu,aliona uovu wa mama yake ambaye alikuwa mhiti(neno Mhiti ni msingi)
Ikiwa Mungu  mwenyewe alikuwa akishughulikia uovu kwenye misingi je! Wewe mtumishi  wa Mungu unashughulikia uovu kutoka kwenye nini?,Mungu hakuona dhambi ya Yerusalem kama dhambi bali aliona kama misingi na akaishughulikia kutoka kwenye misingi.
Watumishi wa Mungu nasi tuchukue hatua ili kujenga misingi upya na Mungu atajulikana na kuonekana kwetu.Mungu alipomaliza kazi ya kuvunja misingi mibaya  alichukua hatua zifuatazo ili kujenga misingi upya:-
Alikata kitovu;kitaalam mtoto anapozaliwa kitovu chake kinakatwa ili atengwe na mama yake ,ishara ya Mungu roho ya asili na kumuingiza katika kusudi lake. Mtumishi wa Mungu unaposhughulikia matatizo kata kitovu cha tatizo ndipo  litaisha.
Aliosha Yerusalem kwa maji ;Maji yalimanisha utakaso na usafi,hii inatufundisha pia tufanye utakaso wa vile tulivyo vitenga kwa kusudi la Mungu maana mandiko yanasema Musa alivitakasa vyombo vyote vya madhabahua (Waebrania9:22).
Kutiwa chumvi;hii inamainisha kuondolewa mapooza kama tunavyoona katika 2Wafalme2:19-22 na pia nikumilikishwa kwenye 2Nyakati13:5
Kuwavisha nguo ;ili manisha kurudisha utukufu walioupoteza kwa sababu ya uovu,kwa sababu mtu akifanya dhambi anapungukiwa na nguvu na utukufu wa Mungu.
 Rum 3:23


Katika hivi vipengele tulivyo viangalia inatuonesha ili kutoka kwenye matatizo mbali mbali ni lazima tushughulikie/tubomoe/tuondoe misingi mibovu na kujenga  misingi mipya kama ilivyo ainishwa katika Yeremia1:10 anasema; angalia nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya ufalme ili kungoa na kubomoa na kuharibu na kuangamiza ili kujenga na kupanda;kuanzia sasa mtumishi wa Mungu anza kubomoa misingi yote mibovu katika maeneo yote yanayokubalika na Mungu ataonekana kwako kwa upya. Yesu alipowateua wanafunzi kumi na mbili alikuwa anrejea kwenye msingi.
Hii inatufundisha hivi;kila unachohitaji kujenga cha kimungu ni lazima usimamie kwenye msingi ili kipate kusimama.

Huwezi kuelewa kwa nini alichagua wanafunzi kumi na mbili na sio zaidi,kama hujajua namba kumi na mbili inamana gani katika msingi wa kimungu.
(i)Msingi uliojengwa na Yesu.
Msingi huu aliujenga Yesu alirejea kwa kabila kumi na mbili za Yakobo aliyejiliwa na neno la Bwana na kuambiwa hutaitwa Yakobo ila utaitwa `Israel', na sio Yesu peke yake alierejea kwenye msingi bali hata manabii wengine kama tunavyowaona hapa; “Basi Musa akayaandika maneno yote ya Bwana akaondoka asubuhi na mapema akajenga madhabahu ya Bwana  chini ya mlima na nguzo kumi na mbili kwa hesabu ya kabila kumi na mbili za Israel”
   Kutoka24:4.


(ii)Eliya arejea kwenye Misingi.
Mwingine  alirejea kwenye msingi ni Elia kama anavyoelezwa hapa; “Kisha Elia akawaambia watu wote  nikaribieni mimi ,watu wote wakamkaribia akatengeneza madhabahu ya Bwana iliyoharibika,Elia akatwaa mawe kumi na mbili kwa hesabu ya kabila za wana wa Yakobo aliyejiliwa na neno la BWANA  akaambiwa akambiwa jina lako litakuwa `Israel...' 
 1Wafalme18:30-31


(V).Tumejengwa juu ya Msingi wa Mitume na Manabii na Yesu Kristo ndiye Jiwe kuu la pembeni.
Maana Biblia inasema ninyi nanyi kama mawe yaliyo hai mmejengwa muwe nyumba ya Roho na Yesu akiwa ni jiwe kuu la pembeni  kama maandiko yasemavyo,
''Ninyi nanyi,kama mawe yaliyo hai,mmejengwa muwe nyumba ya Roho,ukuhani mtakatifu,mtoe dhabihu za roho,zinazokubali na Mungu,kwa njia ya Yesu Kristo.Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko;Tazama,naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni,teule,lenye heshima na kila amwaminiye hatatahayarika''.          
1Petro 16:1-4


Maandiko mengine yanaeleza Yesu kuwa jiwe la Msingi.

-Kuna msisitizo kwenye Msingi ndio maana imetajwa mara nyingi.
Maandiko pia yanaendelea kufafanua kua sisi tumejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii.
(i)Mbingu zimejengwa kwenye Msingi.
Mbingu nazo zimejengwa katika msingi.
"Ulikuwa na ukuta mkubwa,mrefu,wenye milango kumi na miwili,na katika ile milango malaika kumi na wawili;na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za waisraeli.Upande wa mashariki milango mitatu;upande wa kaskazini milango mitatu;na upande wa kusini milango mitatu;na upande wa magharibi milango mitatu.Na ukuta wa pili ulikua na milango kumi na miwili,na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo"
Ufunuo 21:12-14


(ii).Faida za kujenga kwenye Msingi wa Yesu Kristo.
Yesu ni msingi kila anayejenga juu ya Yesu kazi yake itasimama,maandiko yanasema;
"Maana msingi mwingine hakuna mtu anayeweza kuuweka isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa yaani Yesu Kristo,kazi ya mtu aliejenga juu ya huu msingi ikikaa utapata thawabu bali ikiteketea utapata hasara..."
1Korintho 3:9-14


"Nisikilezi,ninyi mnaomtafutia haki;nanyi mnaomtafuta Bwana;uangalieni kwamba ule ambao mlitolewa kwa kuchongwa,na tundu la shimo ambalo mlitolewa kwa kuchimbuliwa(Msingi)"
Isaya 51:1


"Wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho;kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata;na mwamba ule ulikua ni Kristo(Msingi)"
1Korintho 10:4


"Bwana akasema,Tazama hapa pana mahali karibu nami,nawe utasimama juu ya mwamba;kisha itakuwa wakati unapopita utukufu wangu,nitakutia katika ufa wa ule mwamba,na kukufunika kwa mkono wangu hata nitakapokuwa nimekwisha kupita.
Nami nitaondoa mkono wangu,nawe utaniona nyuma yangu,bali uso wangu hautaonekana(Msingi)"
Kutoka 33:21-23


Msingi mwingine,
"Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama,wenye muhuri hii,Bwana awajua walio wake.Na tena,kila atajaye Jina la Bwana na aache uovu....(Msingi)"
2Timotheo 2:19-22


Yesu kumjua mtu huo ni msingi na kil atajaye Jina la Bwana na aache uovu;hapa tunajifunza,tunapotenda dhambi tunaondoka kwenye msingi wa kujulikana kama wana wa Mungu.
"Mimi ndimi Mchungaji mwema;nao walio wangu nawajua,nao walio wangu wanijua mimi(Msingi)"
Yohana 10:14


Yesu ni jiwe la Msingi linaloondoa mauti;hapa tunaona ili kuwa hai lazima tukae kwenye Msingi ambao ni Yesu Kristo.
Isaya 28:15-18


Msingi mwingine imara ni mtu kuyasikia maneno ya Mungu na kuyatenda kama yalivyoainishwa kwenye Mathayo 7:24.
-Watumishi wa Isaka kuchimbua vile visima ilikua ni kurudisha misingi na wewe leo unaweza kurudisha misingi yako kama watumishi wa Isaka walivyofanya katika Mwanzo 26:18-23.


(VI).Mungu ana uwezo wa kuweka Misingi yetu katika mawe mazuri.
Mungu ana uwezo wa kuweka misingi yetu katika mawe mazuri ikiwa tutarudi kwenye Msingi na kumuomba.
Isaya 54:11-13


Kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga maana kazi ya mtu hujaribiwa kwa moto.
-Kazi itakayosimama ni ile iliyoko kwenye Msingi wa Yesu.

(i)Msingi wako umeuweka wapi?
Hili ni swali la kujiuliza kila mmoja wetu.
Swali:-
Msingi wako umeweka wapi? Au unaishi katika misingi ya aina gani?
Yamkini umeteseka kwa ajili ya Misingi,pengine Biashara,Ndoa,Huduma,Elimu,Uzima,Watoto,Afya yako na vyote hivyo vina shida kutokana na Msingi uliojenga.
(VII).Hatua za kuchukua ili kurejesha Misingi iliyoharibika.
Sasa unaweza kuchukua Hatua zifuatazo ili kurejesha Misingi iliyoharibika;
-Toba ya kweli.
i. Ingia kwenye toba,na toba hio itakuhusisha wewe na ukoo wako,wazazi wako wawili(Baba na Mama),nchi yako na mahali pa huduma na chochote unachofanya.
Waweza kusimama na maneno haya:
Danieli 9:4
Zaburi 51:1-19
2Nyakati 7:14
Yakobo 5:14-16

-Bomoa Misingi yote iliyopandwa ndani ya Maisha yako.
ii. Vunga misingi mibovu katika maneno yote uliotubia.
Simama katika maandiko haya:
Yeremia 1:10
Yeremia 51:20

-Omba;rejesha misingi yote ya Baraka maishani ili uweze kusonga mbele.
iii.  Fanya maombi  ya kurudisha misingi yako ya kufanikiwa.
Zakaria 9:11-12
Isaya 45:2-3
Isaya 42:18-22
Mwanzo 26:18.

MUNGU AKUTIE NGUVU!!



                                        Imeandaliwa na
                                     Rev.Liberty Shirima
                               Mchungaji Kiongozi(KPYM)
                       +255(0) 756 636 561 / (0) 784 364 561
                             Email: kp.yerusalem@gmail.com

Friday, August 15, 2014

HISTORIA YA KANISA



·         Kanisa  lilianza mwaka elfu mbili na tano(2005), ikiwa kama fellowship ilikuwa ikifanyikia nyumbani kwa  Mr Eustadhi- Bwaize huku ikiwa na  washirika wanne.
·         Baadaye tulifanikiwa  kupata kiwanja cha kukodi,tukajenga jengo la muda la miti. Mwaka elfu mbili na sita (2006) mwezi wa saba hadi elfu mbili na tisa (2009) tulifanikiwa kununua kiwanja cha kanisa,tukahamia rasmi kwenye kanisa hilo mwaka elfu mbili na kumi (2010) mwezi wa kumi, kwa kujenga jengo la muda la miti huku tukiendelea na ujenzi wa jengo la kudumu la kanisa.Mpaka hapo washirika walizidi kuongezeka kutoka wane hadi hamsini(4 – 50).

·         Ilipofika  mwaka elfu mbili na kumi tatu(2013) mwezi wa saba ndipo tulipokamilisha ujenzi wa jengo la kudumu la kanisa likiwa na washirika zaidi ya mia mbili.

MAFANIKIO YA KANISA.


       ·         Kanisa  lilianza mwaka elfu mbili na tano(2005), ikiwa kama fellowship                    ilikuwa ikifanyikia nyumbani kwa  Mr Eustadhi- Bwaize huku ikiwa na                  washirika wanne.

·         Baadaye tulifanikiwa  kupata kiwanja cha kukodi,tukajenga jengo la muda la miti. Mwaka elfu mbili na sita (2006) mwezi wa saba hadi elfu mbili na tisa (2009) tulifanikiwa kununua kiwanja cha kanisa,tukahamia rasmi kwenye kanisa hilo mwaka elfu mbili na kumi (2010) mwezi wa kumi, kwa kujenga jengo la muda la miti huku tukiendelea na ujenzi wa jengo la kudumu la kanisa.Mpaka hapo washirika walizidi kuongezeka kutoka wane hadi hamsini(4 – 50).
·         Ilipofika  mwaka elfu mbili na kumi tatu(2013) mwezi wa saba ndipo tulipokamilisha ujenzi wa jengo la kudumu la kanisa likiwa na washirika zaidi ya mia mbili.



SHUHUDA MBALIMBALI.


  1.  Wagonjwa wengi wamepokea uponyaji
  2.   Watu kuiniliwa kiuchumi
  3.   Watu kuinuliwa kielimu
  4.    Watu kuinuliwa kiroho
  5.   Watu kukombolewa kutoka kwenye nguvu za giza

CHANGAMOTO.

                               
Tumekabiliana na changamto nyingi sana kama vile;
·         Kupigwa vita kwa habari ya mikutano
·         Kupigwa vita kwa habari ya semina,pamoja na ratiba mbali mbali za maombi zilizokuwa zikiendelea hapa kanisani
·         Kupigwa vita na watumishi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusemwa  vibaya kwa Mtumishi na kanisa kwa ujumla

·         Lakini mkono wa Bwana ulikuwa pamoja nasi ukitupigania, hatimaye tukazidi kuwa washindi,Jina la Yesu lipewe sifa, Amen.

MAONO NA MALENGO YA KANISA

           
  •          Tunatalajia kufungua Makanisa Inje na ndani ya  Tanzania
  •          Tunatalajia kuwa na kituo cha Redio na televisheni
  •          Tunatazamia kujenga kanisa kubwa lenye uwezo wa kubeba watu takribani  million tatu
  •          Tunatazamia  kufungua shule ambazo zitakuwa zikichukua wanafunzi kuanzia Kindergaten hadi Chuo Kikuu
  •         Tunatazamia kufungua hospitali,vituo vya kulelea watoto yatima na kusaidia watu wasio jiweza
  •          Pia tunatazamia kuwa na Chuo Kikuu cha Biblia
  •          Tunatazamia  kuwa na vyanzo mbalimbali vya Uchumi pamoja na kuwa na Benki zetu wenyewe