KUKOMBOA WAKATI
Maana ya Wakati?
Ø Wakati ni muda uliowekwa kwa ajili ya kutimiza kusudi maalum lililokusudiwa.
·
Kwa
kila jambo kuna majira yake na kila
kusudi lini wakati wake
·
Kila
alichokifanya Mungu na anachokifanya hata sasa kimefichwa kwenye wakati
·
Watu
ambao wako nje ya wakati hawawezi kukutana na mipango.
Ø Kuna nyakati na makusudi yake kama
ifuatavyo:
·
Mhubiri
3:1-8( Ina nyakati zake)
Kuna wakati wa kukaa imara na wokovu tele(Isaya
33:6)
Wakati wa kukaa imara ina maanisha unapokutana na vipingamiza
vikubwa ni wakati wa kukaa imara.
·
Ndio
maana anasema pia;
“Kesheni ,simameni imara
katika imani fanyeni kiume mkawe hodari”.1korintho
16:13
·
Wakati wa
vipingamizi vikali ndipo tunaweza
kuuona wokovu wa Mungu tele.
Kuna wakati wa kuamka usingizini
·
Warumi
13:11-14
·
1thesalonike
5:1-11
·
Ezekiel
23:3
·
Isaya
60:1
Kuna
wakati wa kuamka
usingizini
·
Yohana
4:20-25
·
Isaya
49:8
·
2koritho
Kuna wakati wa
kujiliwa
·
Luka
19:41-46
·
Malaki3:1-6
·
Ebrania
10:37-39
Ø Kuna ujio wa aina nyingi na kila ujio unakuja kwa wakati wake
Kuna
wakati wa kujenga nyumba ya Mungu
·
Hagai
1:2
Ø Kuna wakati upendezao ni
wakati Mungu anapopatikana
·
Zaburi
32:6
·
Pia
Bibilia inasema mtafuteni
Bwana maadam anapatikana
Isaya55:6-7
·
Petro
alienda hekaluni saa 9 ya
kusali ndipo Mungu akamtokea na kumpa uwezo na kumpa uwezo wa
kumponya kiwete.
Matendo3:1
·
Tunapoomba kwa
wakati ndipo Mungu anapoweza kuwa
pamoja nasi.
Ø Kuna chakula cha wakati
·
Mathayo
24:45
·
Luka
12:44-48
·
Mungu
anapenda watumishi wanaowahubiri washirika
neno la wakati
·
Chakula cha
wakati kinapatikana barazani
pa Bwana
Yeremia23:18
·
Ili kupata
chakula cha wakati
kinapatikana ni lazima tumwombe
Mungu atupatie.
Ø Kuna wakati ufaao
kula.
·
Katika
matatizo yanayowakabili watu wengi,miongoni mwa matatizo
yanatokana na kutokula wakati
unaofaa.
·
Kuna nyakati zinazofaa kula na zisizofaa kula.Mfano;
-Wakati wa kufunga si wakati wa kula
-Wakati umebeba jambo mwili unakuhimiza
kufunga kwa ajili ya uzito
wa hilo jambo
-Kuna wakati
ambao mtu unasikia kula
sana unapaswa kula sana
-Kuna muda uliowekwa maalum
kwa ajili ya kula, kwa mfano hapa kwetu
Afrika muda wa kula ni kati ya saa sita
hata saa saba unapokula nje ya hiyo mida unapokula muda
usiofaa.
-Hata kula
kinachotakiwa kuliwa kwa wakati hiyo nayo ni kanuni, hupaswi kula nyama
wakati mwili unataka maharage.
Ø Kuna wakati wa shetani kupanda magugu katikati ya ngano
·
Mathayo
13:24-30,36-43
·
Shetani
anatumia wakati wa usiku kuleta mapando
kwenye maeneo yetu.
·
Ndio
maana Bibilia inasema kesheni kila wakati.
-Hilo neno kukesha ni
kudumu katika mapenzi ya Mungu kila wakati.
·
Tena
Bibilia inasema msimpe ibilisi nafasi.Efeso4:27
-Kumpa ibilisi nafasi ni
kuachia wakati
-Ndio maana Bibilia
inatumbia tuukumboe wakati,haijasema
tupoteze wakati.
·
Mwenye
kuujua wakati na nyakati ni Yule aliyepo kwenye wakati.
·
Siku
ya kuja Bwana Yesu watakaoijua ni wale
walioshika au waliopo kwenye wakati.
(Danieli12:1-4)
·
Majira
na nyakati za ujio wa Yesu kwa kanisa vimefichwa kwa taifa la Israeli.
(Mathayo24:32-33)
·
Mapango
yote ya Mungu imefichwa katika wakati na
anayeweza kuiona ni Yule anayetembea na wakati.
·
Pia tunaweza kusifahamu nyakati kwa kuvisoma vitabu
(Danieli 9:2-3)
·
Pia tunaweza
kuzifahamu nyakati kwa
ufunuo wa Roho Mtakatifu.(2petro
1:18-210)
Ø Maisha yetu
yamefichwa katika wakati.
(Isaya 26:16-19).
·
Wakati ndio unaobeba
siku za mtu za kuishi hapa
duniani, hivyo anayeweza kuishi
miaka ya ahadi ni Yule anayeishi ndani ya wakati.(yoeli2:12,25).
·
Mungu
anatuesabia siku za kuishi hapa duniani.
·
Tunapofanya dhambi siku zetu kuishi hapa
duniani zinapunguzwa.
-Mithali 10:27
-Mhubiri 7:17
·
Moyo wa mwenye hekima ndio
unaoweza kujua wakati wa kudumu.
·
Wakati
wa mtumishi unapokamatwa mpango ambao Mungu
alimkusudia hapa duniani
unakuwa umekamatwa.Mfano;
-wakati wana wa Israeli ulikamatiwa Misri kwa muda wa miaka mia nne na thelasini(430)
-Wakati wa Yusufu
ulikamatiwa nyumbani kwa Potifa
na gerezani
-Wakati pia wa Yakobo ulikamatwa na
Labani
Swali:
Je wakati wako
umekamatwa na nani?,na je upo kwenye kusudi la Mungu?,kumbuka jambo hili, kama upo kwenye katika wakati wa
Mungu, Mungu anafanya kazi pamoja
wewe?,na ataifanikisha huduma yako kwa viwango vikubwa?,tumwombe Mungu
aturejeshee tena nyakati zetu ili tuweze
kufanikiwa katika yote tuyatendayo.
Imeandaliwa na
Rev.Liberty Shirima
Mchungaji kiongozi(KPYM)
+255(0)756636561/0784364561
Email:kp.yerusalem.gma
SOMO LA PILI LA MAHUSIANO
SOMO LA PILI LA MAHUSIANO
MAHUSIANO
Mahusiano ni nini?
Mahusiano
ni uwiano uliopo kati ya mtu na wengine; na kati ya mtu na Mungu.
Biblia
inasema watu wawili hawawezi kwenda pamoja wasipo patana.
“je watu wawili waweza kutembea
pamoja, wasipokuwa wamepatana?”
Amosi 3:3
Kwa
hiyo tunaweza kusema mahusiano ni mapatano na makubaliano baina watu wawili au
zaidi waliokubaliana na kushilikiana.
A.MAHUSIANO
KATI YA MUNGU NA MWANADAMU
Mungu
ndiye mwanzilishi wa mahusiano huko juu
mbinguni.Kwa mfano: “Mungu akasema na tumfanye mtu kwa sura na mfano
wetu”.Mwanzo 1:27
-Hapa
inaonesha Mungu hakuwa anafanya mwenyewe bali katika ushirika na mahusiano,
angefanya mwenyewe angesema `nafanya mtu' sio 'tumfanye mtu'.
-Hivyo
mahusiano mazuri huko kwa Mungu yalisababisha mambo makubwa kutendeka hususani
uumbaji.
-Muhusiano
haya Mungu yalikuwa katika utatu mtakatifu ambao ni Mungu Baba, Mwana na Roho
mtakatifu.
-Mahusiano
na ushirika wa Mungu katika utatu mtakatifu yalisababisha nchi na vyote
kuumbwa.
-Katika
ufalme wa Mungu mafanikio yote yamefichwa katika mahusiano.
Mungu
alipoumba ulimwengu alimwuumba mtu katika hali ya mahusiano kati ya mtu huyo na
yeye, ndio maana hakumfinyanga mtu huyo
kwa udongo tu ikatosha,bali alimpulizia pumzi puani mwake mtu akawa nafsi hai.
“Bwana Mungu akamfanya mtu mavumbi ya
ardhi,akampulizia pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai”(mwanzo2:7).
Lengo
la kumpulizia pumzi ya uhai puani ni ili kuingiza sura na mfano wake ndani ya
mtu huyo (mwanzo1:26-27)
-Sura
na mfano wa Mungu vinatufundisha kuhusu
mahusiano yaliyowekwa kati ya Mungu wanadamu.
-Mungu
alimuweka mwanadamu katika bustani ya Edeni na awkawa akimtembelea hapo kwa
sababu ya mahusiano aliyokuwa nayo kati yake na huyo mwanadamu.
-Mwanadamu
alipofanya dhambi aliondoka kwenye mahusiano kati yake na Mungu kwa sababu sura
na mfano wa Mungu ambayo ndio sababu ya mahusiano ilikufa,kama tunavyoona
katika kifungu hiki cha maandiko katika Efeso2:1
-Mungu
alipofika bustanini alimwita, Adam! Adam! Adam! Uko wapi?...Adam akajibu,
“nimesikia sauti yako bustanini nikaogopa nikajificha maana mimi ni
uchi...”,kilichosababisha wasijione uchi wao kabla ya kufanya dhambi ni
mahusiano waliyokuwa nayo na Mungu(ambayo
ni sura na mfano wake).
-Hii
inatufundisha kuwa tunapofanya dhambi utukufu wa Mungu uliokuwa umetufunika
unaondoka kwa sababu sura na mfano wa
Mungu vimeondoka.
-Hivyo Mungu alipomwita Adam na kumuuliza uko wapi Adam ni kwa sababu
amemkosa kwenye mahusiano.
-Tunakataliwa
na Mungu kwa sababu ya kuondoka kwenye mahusiano.
“Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;
kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa,mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umesahau sheria
ya Mungu wako,mimi nami nitawasahau watoto wako”(Hosea4:6).
Hapa
Mungu anaongea maneno magumu kwamba tukiondoka kwenye mahusiano sii tu
kwamba tutaathirika peke yetu bali hata
vizazi vyetu vitaathirika,tunapaswa
tulinde sana mahusiano yetu na Mungu ili tuokolewe na vizazi vyetu
vilivyopo na vijavyo.
B: MAHUSIANO KATI YA
WANADAMU
Katika
kutengeneza mahusiano Mungu alianza mahusiano katika ndoa kama ilivyoainishwa
katika kifungu kifuatacho cha mandiko
“Bwana
Mungu akasema, si vyema huyo mtu awe
peke yake nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye”(mwanzo 2:18).
Hilo
neno `kufanana naye` linamaanisha
mahusiano kati mke na mume ambao ni
wanandoa na si vinginevyo.
a)
Ndoa
Mahusiano
ya kwanza ambayo Mungu aliyatengeneza kati ya wanadamu ni mahusiano ya wanandoa.
Ndoa maana yake nini?
Ndoa
ni muunganiko wa hiari baina ya mwanamke
na mwanamme wenye nia ya kudumu maisha yao yote.
·
Kuna mahusiano yaliyowekwa
kati ya wanandoa yanayoleta
Baraka(mathayo 21:19).
·
Kuna mahusiano yaliyowekwa kati ya watu na watu pia yakaleta
Baraka(zaburi 133:1-3).
·
Kuna mahusiano kati ya Mungu na wanadamu pia yanaleta
Baraka(Rum 8:28).
·
Kuna mahusiano katia mwanadamu na ardhi yanayoleta
Baraka(Hosea2:21-23).
·
Kuna mahusiano kati ya wachungaji na wachungaji yanayoleta
Baraka(Yohana17:22).
·
Kuna mahusiano kati ya
waajiri na waajiriwa wao yanayoleta Baraka(Efeso 6:5-9).
·
Kuna mahusiano kati ya wazazi na watoto wao yanayoleta
Baraka(Efeso 6:41-4).
Hivyo kulingana na vifungu tulivyoviangalia ni
wazi kabisa ikiwa tutasimama katika
mahusiano sahihi ni lazima tuzione Baraka za Mungu.Yesu akasema wawili wenu ama
watatu wakipatana kwa jambo lolote duniani watafanyiwa na Baba aliye mbinguni.
·
Neno lile `wawili wenu` kwa maana nyingine linamaanisha
wanandoa.
·
Neno`watatu` linamaanisha kanisa.Mathayo18:19-20 .Yesu akasema
ndugu zangu na jamaa zangu ni wale wanao yasikia maneno ya Mungu na kuyatenda.
·
Hii inaonyesha tunaposikia maneno ya Mungu na kuyatenda
tuimalisha mahusiano yetu na Yesu(mathayo12:46-50),ndio maana pia Yesu anasema yeye aliye na amri zangu na kuzishika yeye ndiye
anipendaye na yeye anipendaye atapendwa
na Baba yangu nami nitampenda na
kujidhihirisha kwake(yohana14:21).
·
Kule kujidhirisha ni ishara ya mahusiano
maana ni kuonekana au tunaweza kusema kujifununua katikati yetu yetu tunapokuwa
na mahusiano mazuri.Katika mithali 8:17
Mungu anasema”nawapenda wale wanipendao.....”.
·
Hii inaonyesha
tusipokuwa na mahusiano mazuri na Mungu,Mungu hawezi kuwa na mahusiano mazuri
na sisi.Mungu anasema nimemuona Daudi aliyeupendeza moyo wangu.
“Nimefanya
agano na mteule wangu, nimemuapia Daudi,mtumishi wangu”(zaburi89:3). Mstari wa
20 unaendelea kusema “Nimemwona
Daudi,mtumishi wangu nimempaka mafuta yangu matakatifu”.
Mstari wa
27-28 unasema; “Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wa kwanza ,kuwa juu
sana kuliko wafalme wa dunia.Hata milele nitamwekea fadhili zangu, na
agano langu litafanyika amini
kwake”.Kilichosababisha Mungu kumuona Daudi ni mahusiano mazuri aliyokuwa nayo
na Mungu.Kila eneo na kila mahali kinachosababisha mtu apate mema ni mahusiano
aliyo nayo hapo mahali na kwa hao
watu,kwa mfano;
·
Mtu mwenye mahusiano mazuri
na Mungu atapokea Baraka za Mungu.
·
Mchungaji mwenye
mahusiano mazuri na As kofu wake atapokea mema kutoka kwake.
·
Mshirika mwenye mahusiano mazuri na mchungaji wake atapata
mema kutoka kwa mchungaji wake.
·
Kadhalika mtoto mwenye mahusiano mazuri na wazazi wake atapokea mema kutoka kwa
wazazi wake. Tukiwa na mahusiano na
Mungu kama Baba tutapata kibali cha
kumwomba na hivyo tutapokea mahitaji yetu toka kwake kama tunavyoona katika
vifungu hivi; ``Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni,jina lako
litukuzwe,ufalme wako uje`` (Mathayo 6:9).Yesu hakusema ombeni mseme Mungu wetu
uliye mbinguni bali aliwaambia waseme BABA YETU ULIYE MBINGUNI.Kwa
nini alisema Baba yetu aliye
mbinguni?..anamaanisha mahusiano tuliyonayo na Mungu kama Baba yanasababisha kupokea majibu ya maombi kutoka
kwake.
Angalizo:- kama Mungu sio Baba kwako uruhusiwi kusali sala ile
ya `Baba yetu uliye mbinguni`, “Bali
waliompokea aliwapa uwezo uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu,ndio wale
waliaminio jina lake”(yohana 1:12).
Hii ni wazi
kwamba kama Mungu si Baba kwako usimwombe maana hutapata chochote kutoka
kwake.Mungu anashika maagano na Rehema kwa wampendao.
“Nikamwona Bwana,Mungu
wangu,nikaungama,nikasema,Ee Bwana,Mungu Mkuu,mwenye kutisha,ashikaye maagano
na rehema kwao wampendao,na kuzishika amri zake.”(Daniel9:4)
Swali; je!! Una sifa za kusababisha Mungu ashaghulike na
mahitaji yako?.Mungu akasema huyu ni mwanangu mpendwa msikilizeni yeye “5
alipokuwa katika kusema,tazama,wingu jeupe likawatia uvurli; na tazama,sauti
ikatoka katika lile wingu,ikasema,huyu ni mwanangu mpendwa wangu,ninayependezwa
naye;msikilizeni yeye..``(mathayo17:1-7)
Inamaanisha
mahusiano yaliyo kuwepo kati Yesu na Mungu yalisababisha awe mwana mpendwa na
mwenye uwezo wa kumkaribia Mungu na Mungu akajifunua kwake.
Kwa mfano kuna
mahusiano ya kirafiki kati yetu na Yesu.
“Ninyi mmekuwa
rafiki zangu,mkitenda niwaamuruyo.Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui
atendalo bwana wake lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa niliyoyasikia kwa
Baba yangu nimewaarifu.
-
Kilichosababisha Lazaro kufufuliwa ni mahusiano mazuri ya
kirafiki yaliyokuwepo kati ya Mariam ,Martha,Lazaro na Yesu.Yoh 11:2,3,35-38
Swali-Je! Yesu ni rafiki
kwako?
-Abrahamu alikuwa na mahusiano ya karibu sana na Mungu kuliko
mke wake na Mungu akamuinua.
Mwanzo 22:1-14
Hii inamaanisha mtu yeyote mwenye mahusiano
mazuri na Mungu lazima amtii Mungu na
anapomtii Mungu ni lazima afanikiwe.
-
Musa alikuwa na mahusiano mazuri na Mungu kuliko Haruni
na Miriam ndio maana Mungu akajifunua kwa Musa kuliko Haruni na Miriam.
Hesabu 12:1-8
Hapa tunaendelea kuona
kiwango kikubwa cha mahusiano kinavyosababisha Mungu kujifunua kwetu kwa kiwango kikubwa.
B :MAHUSIANO NA
WANADAMU
Mwanzo wa uumbaji
wa Mungu akamuumba mtu mume
akamfanyia msaidizi wa kufanana
naye; tafsiri nyingine inasema wakumfaa.(mwanzo2:18)
Hii inatufundisha
mahusiano ambayo Mungu alianzisha kwa wanadamu wawili
Tusipokuwa
na mahusiano tunakuwa tumejiondoa kwenye mpango wa Mungu
Bibilia inaweka wazi
kuwa kanisa la kwanza walimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote ndipo Bwana
akalizidisha
kanisa.(mtendo2:43-47)
Kuwapendeza watu
wote inamaanisha mahusiano
baina yao na watu
wengine.Hii inamaana huduma
yeyote ambayo haina mahusiano mazuri na watu haiwezi kufanikiwa
swali; je! Mahusiano kati
yako ,huduma yako na wale wanao kuzunguka ikoje?
C)mahusiano
ya watumishi na wa Anaowaongoza
Hapa tunajifuza kwa
watumishi wa Mungu,Paulo
alipokuwa akiwaambia watakatifu wa kanisa la Koritho tupeni nafasi
mioyoni mwenu.Lile neon nafasi ni mahusiano.
``tupeni nafasi mioyoni mwenu,
hatukumdhulumu mtu yeyote, wala kumharibu, wala kumkaramikia
mtu``.(2koritho7:2)
Hii inatufundisha
watumishi wa Mungu lazima tujenge mahusiano
mazuri kati yetu na wale
tunaowaongoza ili sisi pamoja na
huduma tulizo nazo tupate nafasi na
kibali mioyoni mwao.Bibilia pia inatuasa
tusijipendeze wenyewe bali tuwapendeze na wengine ili tupate wema
tukajengwe.(Rum15:1-5)
Hii inatuonesha
wazi kujengwa kwetu kuna sababishwa na
mahusiano tuliyonayo ya kuwapendeza pia wengine. Mandiko yanatuambia pia Yesu
alikuwa katika hekima na kimo
akimpendeza Mungu na wanadamu luka2:52
Swali:-Je! mahusiano yako na jamii kama mtumishi ni ya
kiwango gani?
Hii
inatufundisha kumpenda Mungu lakini hawawapendi wanadamu wenzao. Bibilia pia
inasema mtu atasemaje anampenda Mungu asiyemwona huku anamchukia ndugu yake
anayemwona?.
Mahusiano
mazuri na watu wengine yanasababisha Baraka za Mungu kwetu kutokana na hao watu.
·
Huduma ni watu hivyo kuharibu watu ni kuharibu huduma, kuna
mifano mingi inayoonyesha watu waliobarikiwa katika mahusiano yao na watu.
1.
Sulemani (watu walimletea utajiri)
2.
Yesu (watu walimhudumia
kwa mali zao) (Luka 8:1-4)
3.
Eliya (Mwanamke wa serepta alimlisha)
4.
Elisha (Mwanamke Mshunami alimtunza)
Hivyo hii
inatuonyesha Mungu anatubariki kupitia
watu na watu hawawezi kufanya chochote kwao kama huna mahusiano mazuri
nao.
MUHIMU:
Maaskofu na
Wachungaji tuwe na mahusiano mazuri na tunawaongoza ili wafanyike Baraka kwetu.
Mungu
ametuonya tusiharibu kondoo wa malisho yake.
(Yeremia 23:1-4)
Kama
hatutajenga mahusiano mazuri nae amesema ataweka juu yao wachungaji watakao
walisha, hivyo tutunze sana mahusiano na tunaowaongoza ili Mungu atubariki
maana pia anasema katika Isaya 43:4 ameandaa watu kwa ajili yetu na kabila
za watu kwaajili ya maisha yetu. La
muhimu hapa ni kujua watu ndio Baraka
yetu, hivyo tulinde mahusiano yetu nao ili watubariki.
C. NINI CHA KUFANYA ILI TUWE
NA MAHUSIANO MAZURI NA MUNGU WETU
Ili tuwe na
mahusiano mazuri na Mungu lazima tuzingatie yafuatayo ;
·
Tushike neno la Mungu na kulitendea kazi
·
Tumpende Mungu kwa
mioyo yetu yote na kwa nguvu zetu zote(torati6:5)
·
Tuwe waaminifu mbele za Mungu katika kila jambo
·
Tufanye mapenzi ya Mungu(mathayo7:21)
·
Tujitenge na maovu(2korinto6:14-18).
Ili turudishe mahusiano mazuri lazima
tuondoe wageni kwenye maisha yetu ambao wamechukua nafasi ya Yesu.
`` Ikawa, katika kukaa huko siku zake za kuzaa zikatimia.Akamzaa mwanawe,kifungua
mimba,akamvisha nguo za kitoto,akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe,kwa sababu
hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni’’(luka2:6-7)
Yamkini kuna wageni wanaomzuia Yesu
kuamua kwenye maisha yako inatupasa
uwaondoe,umkaribishe Yesu na ufanye
mahusiano nae ndipo utapomwona
akishughulika nawe.Wageni wanaweza kuwa
liturugia uliyonayo,kiburi cha elimu,kiburi cha mali na vyote vinavyoweza kuushika moyo wako hivyo ni wageni unapaswa uwaondoe. Yesu
anamaliza katika ufunuo 3:20 na kusema;
`` Tazama nasimama mlangoni na
nabisha; mtu akisikia sauti yangu na kufungua mlango,nitaingia kwake,nami
nitakula pamoja naye,naye pamoja name’’
Mkaribisheni Yesu leo ili afanye jambo jipya kakika maisha yako,huduma,na kila
unachohitaji.
Imeandaliwa na
Rev.Liberty
Shirima
Mchungaji
kiongozi(KPYM)
+255(0)756636561/(0)784364561
Email:kp.yerusalem@gmail.com
No comments:
Post a Comment