MAFUNDISHO/MASOMO

                        KUKOMBOA  WAKATI
                                      Maana  ya Wakati?
Ø Wakati ni muda uliowekwa kwa ajili ya kutimiza kusudi maalum       lililokusudiwa.
·        Kwa kila  jambo kuna majira yake na kila kusudi lini wakati wake
·        Kila alichokifanya Mungu na anachokifanya hata sasa kimefichwa kwenye wakati
·        Watu ambao wako nje ya wakati  hawawezi  kukutana na mipango.
Ø Kuna nyakati na makusudi  yake  kama  ifuatavyo:
·        Mhubiri 3:1-8( Ina  nyakati zake)
Kuna  wakati wa kukaa imara na wokovu tele(Isaya 33:6)

Wakati  wa  kukaa imara  ina maanisha unapokutana na vipingamiza vikubwa ni wakati wa kukaa imara.
·        Ndio maana  anasema pia;
“Kesheni ,simameni imara katika  imani fanyeni kiume mkawe hodari”.1korintho 16:13
·        Wakati  wa  vipingamizi  vikali ndipo tunaweza kuuona wokovu wa  Mungu tele.
Kuna  wakati wa  kuamka usingizini
·        Warumi 13:11-14
·        1thesalonike 5:1-11
·        Ezekiel 23:3
·        Isaya 60:1
                                    Kuna wakati  wa  kuamka  usingizini
·        Yohana 4:20-25
·        Isaya 49:8
·        2koritho
Kuna wakati wa  kujiliwa
·        Luka 19:41-46
·        Malaki3:1-6
·        Ebrania 10:37-39
Ø Kuna ujio wa aina nyingi na kila ujio unakuja kwa  wakati wake
Kuna  wakati wa  kujenga  nyumba ya Mungu
·        Hagai 1:2
Ø Kuna  wakati  upendezao ni  wakati Mungu anapopatikana
·        Zaburi 32:6
·        Pia Bibilia  inasema  mtafuteni  Bwana maadam anapatikana
Isaya55:6-7
·        Petro alienda hekaluni  saa 9  ya  kusali ndipo Mungu akamtokea na kumpa uwezo na kumpa uwezo  wa  kumponya  kiwete.
Matendo3:1
·        Tunapoomba  kwa  wakati ndipo Mungu  anapoweza kuwa pamoja nasi.
Ø Kuna chakula  cha wakati
·        Mathayo 24:45
·        Luka 12:44-48
·        Mungu anapenda watumishi  wanaowahubiri  washirika  neno  la  wakati
·        Chakula  cha  wakati  kinapatikana  barazani  pa Bwana
     Yeremia23:18
·        Ili  kupata  chakula  cha  wakati  kinapatikana  ni  lazima  tumwombe  Mungu  atupatie.
Ø Kuna  wakati  ufaao  kula.
·        Katika matatizo yanayowakabili  watu  wengi,miongoni  mwa matatizo  yanatokana  na kutokula  wakati  unaofaa.

·        Kuna  nyakati zinazofaa  kula na zisizofaa kula.Mfano;

-Wakati  wa kufunga si wakati  wa kula
-Wakati  umebeba jambo mwili  unakuhimiza  kufunga  kwa ajili  ya uzito  wa hilo  jambo
-Kuna  wakati  ambao mtu  unasikia  kula  sana  unapaswa kula sana
-Kuna  muda uliowekwa  maalum  kwa ajili ya kula, kwa mfano hapa kwetu  Afrika  muda  wa kula ni kati ya saa  sita  hata  saa saba unapokula nje  ya hiyo mida unapokula  muda  usiofaa.
-Hata  kula  kinachotakiwa  kuliwa  kwa wakati hiyo nayo ni kanuni, hupaswi  kula nyama  wakati mwili unataka maharage.
Ø Kuna  wakati wa shetani  kupanda magugu  katikati ya ngano
·        Mathayo 13:24-30,36-43
·        Shetani  anatumia wakati wa usiku kuleta mapando kwenye maeneo yetu.
·        Ndio maana Bibilia inasema kesheni kila wakati.
-Hilo neno kukesha ni kudumu katika mapenzi ya Mungu kila wakati.
·        Tena Bibilia inasema msimpe ibilisi nafasi.Efeso4:27
-Kumpa ibilisi nafasi ni kuachia wakati
-Ndio maana Bibilia inatumbia tuukumboe wakati,haijasema  tupoteze  wakati.
·        Mwenye kuujua wakati na nyakati ni Yule aliyepo kwenye wakati.
·        Siku ya kuja Bwana Yesu  watakaoijua ni wale walioshika au waliopo kwenye wakati.
(Danieli12:1-4)
·        Majira na nyakati za ujio wa Yesu kwa kanisa vimefichwa kwa taifa la Israeli.
(Mathayo24:32-33)
·        Mapango yote ya Mungu imefichwa katika  wakati na anayeweza kuiona ni Yule anayetembea na wakati.
·        Pia  tunaweza kusifahamu  nyakati kwa kuvisoma  vitabu
   (Danieli 9:2-3)
·        Pia  tunaweza  kuzifahamu  nyakati  kwa  ufunuo wa Roho  Mtakatifu.(2petro 1:18-210)
Ø   Maisha  yetu  yamefichwa  katika  wakati.
                    (Isaya 26:16-19).
·        Wakati  ndio unaobeba  siku za mtu  za  kuishi hapa  duniani, hivyo anayeweza  kuishi miaka ya ahadi ni Yule anayeishi ndani ya wakati.(yoeli2:12,25).
·        Mungu anatuesabia siku  za kuishi hapa  duniani.
·        Tunapofanya  dhambi siku zetu kuishi  hapa  duniani zinapunguzwa.
-Mithali 10:27
-Mhubiri 7:17
·        Moyo  wa mwenye hekima  ndio  unaoweza  kujua  wakati wa kudumu.
·        Wakati wa mtumishi unapokamatwa mpango ambao Mungu  alimkusudia  hapa  duniani  unakuwa  umekamatwa.Mfano;
-wakati  wana wa Israeli  ulikamatiwa Misri  kwa muda wa miaka mia nne na thelasini(430)
-Wakati  wa Yusufu  ulikamatiwa  nyumbani kwa  Potifa  na  gerezani
-Wakati   pia wa Yakobo  ulikamatwa na  Labani



Swali:
Je  wakati wako umekamatwa na nani?,na je upo kwenye kusudi la Mungu?,kumbuka  jambo hili, kama upo kwenye katika wakati wa Mungu, Mungu anafanya  kazi pamoja wewe?,na ataifanikisha huduma yako kwa viwango vikubwa?,tumwombe Mungu aturejeshee tena nyakati  zetu ili tuweze kufanikiwa katika yote tuyatendayo.




                   Imeandaliwa na
                 Rev.Liberty Shirima
           Mchungaji  kiongozi(KPYM)
    +255(0)756636561/0784364561
        Email:kp.yerusalem.gma


     SOMO LA PILI   LA                     MAHUSIANO


               MAHUSIANO
Mahusiano ni nini?
Mahusiano ni uwiano uliopo kati ya mtu na wengine; na kati ya mtu na Mungu.
Biblia inasema watu wawili hawawezi kwenda pamoja wasipo patana.
“je watu wawili  waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?
                Amosi 3:3
Kwa hiyo tunaweza kusema mahusiano ni mapatano na makubaliano baina watu wawili au zaidi waliokubaliana na kushilikiana.
 A.MAHUSIANO KATI YA MUNGU NA MWANADAMU
Mungu ndiye mwanzilishi wa mahusiano huko  juu mbinguni.Kwa mfano: “Mungu akasema na tumfanye mtu kwa sura na mfano wetu”.Mwanzo 1:27
-Hapa inaonesha Mungu hakuwa anafanya mwenyewe bali katika ushirika na mahusiano, angefanya mwenyewe angesema `nafanya mtu' sio 'tumfanye mtu'.
-Hivyo mahusiano mazuri huko kwa Mungu yalisababisha mambo makubwa kutendeka hususani uumbaji.
-Muhusiano haya Mungu yalikuwa katika utatu mtakatifu ambao ni Mungu Baba, Mwana na Roho mtakatifu.
-Mahusiano na ushirika wa Mungu katika utatu mtakatifu yalisababisha nchi na vyote kuumbwa.
-Katika ufalme wa Mungu mafanikio yote yamefichwa katika mahusiano.
Mungu alipoumba ulimwengu alimwuumba mtu katika hali ya mahusiano kati ya mtu huyo na yeye, ndio maana hakumfinyanga  mtu huyo kwa udongo tu ikatosha,bali alimpulizia pumzi puani mwake mtu akawa nafsi hai.
       “Bwana Mungu akamfanya mtu mavumbi ya ardhi,akampulizia pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai”(mwanzo2:7).
Lengo la kumpulizia pumzi ya uhai puani ni ili kuingiza sura na mfano wake ndani ya mtu huyo (mwanzo1:26-27)
-Sura na mfano wa Mungu vinatufundisha  kuhusu mahusiano yaliyowekwa kati  ya Mungu  wanadamu.
-Mungu alimuweka mwanadamu katika bustani ya Edeni na awkawa akimtembelea hapo kwa sababu ya mahusiano aliyokuwa nayo kati yake na huyo mwanadamu.
-Mwanadamu alipofanya dhambi aliondoka kwenye mahusiano kati yake na Mungu kwa sababu sura na mfano wa Mungu ambayo ndio sababu ya mahusiano ilikufa,kama tunavyoona katika kifungu hiki cha maandiko katika Efeso2:1
-Mungu alipofika bustanini alimwita, Adam! Adam! Adam! Uko wapi?...Adam akajibu, “nimesikia sauti yako bustanini nikaogopa nikajificha maana mimi ni uchi...”,kilichosababisha wasijione uchi wao kabla ya kufanya dhambi  ni mahusiano waliyokuwa nayo  na Mungu(ambayo ni sura na mfano wake).
-Hii inatufundisha kuwa tunapofanya dhambi utukufu wa Mungu uliokuwa umetufunika unaondoka kwa sababu  sura na mfano wa Mungu vimeondoka.
-Hivyo  Mungu alipomwita  Adam na kumuuliza uko wapi Adam ni kwa sababu amemkosa kwenye mahusiano.
-Tunakataliwa na Mungu kwa sababu ya kuondoka kwenye mahusiano.
  “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa,mimi nami nitakukataa wewe, usiwe  kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umesahau sheria ya Mungu wako,mimi nami nitawasahau watoto wako”(Hosea4:6).
Hapa Mungu anaongea maneno magumu kwamba tukiondoka kwenye mahusiano sii tu kwamba  tutaathirika peke yetu bali hata vizazi vyetu vitaathirika,tunapaswa  tulinde sana mahusiano yetu na Mungu ili tuokolewe na vizazi vyetu vilivyopo na vijavyo.
                   

 B: MAHUSIANO KATI YA WANADAMU

Katika kutengeneza mahusiano Mungu alianza mahusiano katika ndoa kama ilivyoainishwa katika kifungu kifuatacho cha mandiko
“Bwana Mungu akasema, si vyema  huyo mtu awe peke yake nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye”(mwanzo 2:18).
Hilo neno `kufanana naye` linamaanisha mahusiano kati mke na mume ambao ni  wanandoa na si vinginevyo.
a)    Ndoa
Mahusiano ya kwanza ambayo Mungu aliyatengeneza kati ya wanadamu ni mahusiano ya  wanandoa.
           
                    Ndoa maana yake nini?
Ndoa ni muunganiko wa hiari  baina  ya mwanamke  na mwanamme wenye nia ya kudumu maisha yao yote.
·       Kuna mahusiano yaliyowekwa  kati ya wanandoa  yanayoleta Baraka(mathayo 21:19).
·       Kuna mahusiano yaliyowekwa kati ya watu na watu pia yakaleta Baraka(zaburi 133:1-3).
·       Kuna mahusiano kati ya Mungu na wanadamu pia yanaleta Baraka(Rum 8:28).
·       Kuna mahusiano katia mwanadamu na ardhi yanayoleta Baraka(Hosea2:21-23).
·       Kuna mahusiano kati ya wachungaji na wachungaji yanayoleta Baraka(Yohana17:22).
·       Kuna mahusiano kati ya  waajiri  na waajiriwa  wao yanayoleta Baraka(Efeso 6:5-9).
·       Kuna mahusiano kati ya wazazi na watoto wao yanayoleta Baraka(Efeso 6:41-4).
 Hivyo kulingana na vifungu tulivyoviangalia ni wazi kabisa  ikiwa tutasimama katika mahusiano sahihi ni lazima tuzione Baraka za Mungu.Yesu akasema wawili wenu ama watatu wakipatana kwa jambo lolote duniani watafanyiwa na Baba aliye mbinguni.
·       Neno lile `wawili wenu` kwa maana nyingine linamaanisha wanandoa.
·       Neno`watatu` linamaanisha kanisa.Mathayo18:19-20 .Yesu akasema ndugu zangu na jamaa zangu ni wale wanao yasikia maneno ya Mungu na kuyatenda.
·       Hii inaonyesha tunaposikia maneno ya Mungu na kuyatenda tuimalisha mahusiano yetu na Yesu(mathayo12:46-50),ndio  maana pia Yesu anasema yeye  aliye na amri zangu na kuzishika yeye ndiye anipendaye na yeye anipendaye  atapendwa na  Baba yangu nami nitampenda na kujidhihirisha kwake(yohana14:21).
·       Kule kujidhirisha ni ishara ya mahusiano maana ni kuonekana au tunaweza kusema kujifununua katikati yetu yetu tunapokuwa na mahusiano mazuri.Katika  mithali 8:17 Mungu anasema”nawapenda wale wanipendao.....”.
·       Hii  inaonyesha tusipokuwa na mahusiano mazuri  na  Mungu,Mungu hawezi kuwa na mahusiano mazuri na sisi.Mungu anasema nimemuona Daudi aliyeupendeza moyo wangu.
“Nimefanya agano na mteule wangu, nimemuapia Daudi,mtumishi wangu”(zaburi89:3). Mstari wa 20  unaendelea kusema “Nimemwona Daudi,mtumishi wangu nimempaka mafuta yangu matakatifu”.
Mstari wa 27-28 unasema;  “Nami  nitamjalia kuwa mzaliwa wa kwanza ,kuwa juu sana kuliko wafalme wa dunia.Hata milele nitamwekea fadhili zangu, na agano  langu litafanyika amini kwake”.Kilichosababisha Mungu kumuona Daudi ni mahusiano mazuri aliyokuwa nayo na Mungu.Kila eneo na kila mahali kinachosababisha mtu apate mema ni mahusiano aliyo nayo hapo  mahali na kwa hao watu,kwa mfano;
·       Mtu mwenye mahusiano mazuri  na Mungu atapokea Baraka za Mungu.
·       Mchungaji  mwenye mahusiano mazuri na As kofu wake atapokea mema kutoka kwake.
·       Mshirika mwenye mahusiano mazuri na mchungaji wake atapata mema kutoka kwa mchungaji wake.
·       Kadhalika mtoto mwenye mahusiano mazuri  na wazazi wake atapokea mema kutoka kwa wazazi wake. Tukiwa na mahusiano  na Mungu kama Baba  tutapata kibali cha kumwomba na hivyo tutapokea mahitaji yetu toka kwake kama tunavyoona katika vifungu hivi; ``Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni,jina lako litukuzwe,ufalme wako uje`` (Mathayo 6:9).Yesu hakusema ombeni mseme Mungu wetu uliye mbinguni bali aliwaambia waseme BABA YETU ULIYE MBINGUNI.Kwa nini  alisema Baba yetu aliye mbinguni?..anamaanisha mahusiano tuliyonayo na Mungu kama Baba  yanasababisha kupokea majibu ya maombi kutoka kwake.
Angalizo:- kama Mungu sio Baba kwako uruhusiwi kusali sala ile ya  `Baba yetu uliye mbinguni`, “Bali waliompokea aliwapa uwezo uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu,ndio wale waliaminio jina lake”(yohana 1:12).
Hii ni wazi kwamba kama Mungu si Baba kwako usimwombe maana hutapata chochote kutoka kwake.Mungu anashika maagano na Rehema kwa wampendao.
         “Nikamwona Bwana,Mungu wangu,nikaungama,nikasema,Ee Bwana,Mungu Mkuu,mwenye kutisha,ashikaye maagano na rehema kwao wampendao,na kuzishika amri zake.”(Daniel9:4)
Swali; je!! Una sifa za kusababisha Mungu ashaghulike na mahitaji yako?.Mungu akasema huyu ni mwanangu mpendwa msikilizeni yeye “5 alipokuwa katika kusema,tazama,wingu jeupe likawatia uvurli; na tazama,sauti ikatoka katika lile wingu,ikasema,huyu ni mwanangu mpendwa wangu,ninayependezwa naye;msikilizeni yeye..``(mathayo17:1-7)
Inamaanisha mahusiano yaliyo kuwepo kati Yesu na Mungu yalisababisha awe mwana mpendwa na mwenye uwezo wa kumkaribia Mungu na Mungu akajifunua  kwake.
Kwa mfano kuna mahusiano ya kirafiki kati yetu na Yesu.
“Ninyi mmekuwa rafiki zangu,mkitenda niwaamuruyo.Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.

-         Kilichosababisha Lazaro kufufuliwa ni mahusiano mazuri ya kirafiki yaliyokuwepo kati ya Mariam ,Martha,Lazaro na Yesu.Yoh 11:2,3,35-38
Swali-Je! Yesu ni rafiki  kwako?
-Abrahamu alikuwa na mahusiano ya karibu sana na Mungu kuliko mke wake na Mungu  akamuinua.
       Mwanzo 22:1-14
Hii  inamaanisha mtu yeyote mwenye mahusiano mazuri  na Mungu lazima amtii Mungu na anapomtii Mungu ni lazima afanikiwe.
-         Musa alikuwa na mahusiano mazuri na Mungu  kuliko Haruni  na Miriam ndio maana Mungu akajifunua kwa Musa kuliko Haruni na   Miriam.
                           Hesabu 12:1-8
Hapa tunaendelea kuona kiwango kikubwa cha mahusiano kinavyosababisha Mungu  kujifunua kwetu kwa kiwango kikubwa.

    B :MAHUSIANO NA WANADAMU
Mwanzo wa  uumbaji  wa Mungu akamuumba  mtu  mume  akamfanyia  msaidizi wa kufanana naye; tafsiri   nyingine inasema  wakumfaa.(mwanzo2:18)

Hii  inatufundisha  mahusiano  ambayo Mungu  alianzisha kwa wanadamu  wawili
Tusipokuwa na  mahusiano  tunakuwa tumejiondoa  kwenye mpango wa Mungu
Bibilia  inaweka wazi  kuwa  kanisa  la kwanza walimsifu  Mungu na kuwapendeza watu wote ndipo  Bwana  akalizidisha  kanisa.(mtendo2:43-47)
Kuwapendeza   watu  wote  inamaanisha  mahusiano  baina yao na  watu wengine.Hii  inamaana  huduma  yeyote ambayo haina mahusiano mazuri na watu haiwezi kufanikiwa                                                                       swali;  je! Mahusiano kati yako  ,huduma yako na wale wanao kuzunguka  ikoje?                                                                                                                         C)mahusiano ya watumishi   na wa   Anaowaongoza
 Hapa tunajifuza  kwa  watumishi wa Mungu,Paulo  alipokuwa akiwaambia watakatifu wa kanisa la Koritho tupeni nafasi mioyoni mwenu.Lile  neon nafasi  ni mahusiano.
          ``tupeni nafasi mioyoni mwenu, hatukumdhulumu mtu yeyote, wala kumharibu, wala kumkaramikia mtu``.(2koritho7:2)
Hii  inatufundisha  watumishi  wa Mungu  lazima tujenge  mahusiano  mazuri  kati yetu  na wale  tunaowaongoza ili sisi  pamoja na huduma tulizo nazo  tupate nafasi na kibali mioyoni mwao.Bibilia pia inatuasa  tusijipendeze wenyewe bali tuwapendeze na wengine ili tupate wema tukajengwe.(Rum15:1-5)
Hii inatuonesha wazi kujengwa kwetu kuna  sababishwa na mahusiano tuliyonayo ya kuwapendeza pia wengine. Mandiko yanatuambia pia Yesu alikuwa katika  hekima na kimo akimpendeza  Mungu na wanadamu luka2:52

Swali:-Je!  mahusiano yako na jamii kama mtumishi ni ya kiwango gani?
Hii inatufundisha kumpenda Mungu lakini hawawapendi wanadamu wenzao. Bibilia pia inasema mtu atasemaje anampenda Mungu asiyemwona huku anamchukia ndugu yake anayemwona?.
Mahusiano mazuri na watu wengine yanasababisha Baraka za Mungu kwetu kutokana na hao watu.
·       Huduma ni watu hivyo kuharibu watu ni kuharibu huduma, kuna mifano mingi inayoonyesha watu waliobarikiwa katika mahusiano yao na watu.
1.    Sulemani (watu walimletea utajiri)
2.    Yesu (watu walimhudumia  kwa mali zao)    (Luka 8:1-4)
3.    Eliya (Mwanamke wa serepta alimlisha)
4.    Elisha (Mwanamke Mshunami alimtunza)
Hivyo hii inatuonyesha Mungu anatubariki kupitia  watu na watu hawawezi kufanya chochote kwao kama huna mahusiano mazuri nao.

MUHIMU:
Maaskofu na Wachungaji tuwe na mahusiano mazuri na tunawaongoza ili wafanyike Baraka kwetu.
Mungu ametuonya tusiharibu kondoo wa malisho yake.
                       (Yeremia 23:1-4)
Kama hatutajenga mahusiano mazuri nae amesema ataweka juu yao wachungaji watakao walisha, hivyo tutunze sana mahusiano na tunaowaongoza ili Mungu atubariki maana pia anasema katika Isaya 43:4 ameandaa watu kwa ajili yetu na kabila za  watu kwaajili ya maisha yetu. La muhimu hapa ni kujua  watu ndio Baraka yetu, hivyo tulinde mahusiano yetu nao ili watubariki.
C. NINI CHA KUFANYA ILI TUWE NA MAHUSIANO MAZURI NA MUNGU WETU
Ili tuwe na mahusiano mazuri na Mungu lazima tuzingatie yafuatayo ;
·       Tushike neno la Mungu na kulitendea kazi
·       Tumpende  Mungu kwa mioyo yetu yote na kwa nguvu zetu zote(torati6:5)
·       Tuwe waaminifu mbele za Mungu katika kila jambo
·       Tufanye mapenzi ya Mungu(mathayo7:21)
·       Tujitenge na maovu(2korinto6:14-18).
Ili turudishe mahusiano mazuri lazima tuondoe wageni kwenye maisha yetu ambao wamechukua  nafasi ya Yesu.
     `` Ikawa, katika kukaa huko siku zake za kuzaa zikatimia.Akamzaa mwanawe,kifungua mimba,akamvisha nguo za kitoto,akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe,kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni’’(luka2:6-7)
Yamkini kuna wageni wanaomzuia Yesu kuamua  kwenye maisha yako inatupasa uwaondoe,umkaribishe  Yesu na ufanye mahusiano nae ndipo  utapomwona akishughulika nawe.Wageni wanaweza kuwa  liturugia uliyonayo,kiburi cha elimu,kiburi cha mali na vyote  vinavyoweza kuushika moyo wako  hivyo ni wageni unapaswa uwaondoe. Yesu anamaliza katika ufunuo 3:20 na kusema;
   ``  Tazama nasimama mlangoni na nabisha; mtu akisikia sauti yangu na kufungua mlango,nitaingia kwake,nami nitakula pamoja naye,naye pamoja name’’
Mkaribisheni  Yesu leo ili afanye  jambo jipya kakika maisha yako,huduma,na kila unachohitaji.

                              Imeandaliwa na 
                                   Rev.Liberty Shirima
                              Mchungaji kiongozi(KPYM)
                           +255(0)756636561/(0)784364561

                            Email:kp.yerusalem@gmail.com










































No comments:

Post a Comment